Alhamisi, 18 Desemba 2014

mpangokazi wa idara ya uinjilisti na umisheni Mbeya




A.    Jina  la idara
Idara hii inaitwa idara ya Uinjilisti na Umisheni.

B.    Maono ya idara (vission)
Kutoa fursa kwa watu wote walioko ndani na nje ya jimbo la Mbeya kusikia Injili ya Yesu kristo, kwa kuanzisha mtembeo wa upandaji wa makanisa yatakayojizidisha katika kila jamii iliyopo duniani kupitia nyenzo ya  uinjilisiti.
C.    Dira ya idara. (Mission)
Kuhubiri Injili  na kupanda makanisa yenye kujizidisha.
Tunaamini kwamba Injili itahubiriwa kwa haraka pindi tutakapofaulu kuwafanya waamini kuwa wanafunzi na kama kanuni ya mazidisho itafanya kazi;
kila mmoja kufundisha mwingine”  
Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi hayo uwakabidhi watu waaminifu wataka faa kuwafundisha na wengine. (2Tim 2:2)i
Tukifanya  ki-Biblia tunapata matokeo ya kiBiblia.
Dira ya idara hii ni kuhakiskisha kila mwammini wa kanisa la mahali pamoja anajihusisha kikamilifu  na agizo kuu. Kuhamasisha na kutia moyo waaamini kutumbua kwamba agizo kuu linamhusu kila mmoja yeye binafsi na kanisa kwa ujumla.
D.    Kauli lengo
Wakati wa Mavuno ni Sasa.
E.     Andiko la idara
Yohana 4:35
,, “Inueni macho yenu  myatazame mashamba   yakuwa yameshakuwa meupe tayari kwa mavuno”


F.     Malengo ya Idara
Malengo ya idara yamegawanyika katika maeneo mawili ambayo ni
·       Malengo ya jumla (general objecive)
Malengo ya jumla yanaelezea kusudi hasa la kuwepo kwa idara hii na kile kinachpaswa kutekeleza kwa ujumla wake.
·       Malengo mahususi(Spesific objective)
Malengo mahususi yanafafanua malengo ya jumla kwa kuainisha mambo maalumu ambayo ni msingi wa uwepo wa idara hii. Malengo mahususi yanatuwezesha kupata matokeo ya muda mfupi na yenye kupimika .

§  Malengo ya jumla
Idara hii ya uinjilisti na umisheni imeanzishwa kwa kusudi la kuharakisha utekelezaji wa Agizo kuu la Bwana wetu Yesu Kristo.
Akawaambia “Enendeni ulimwenguni mwote mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe” Marko 16:14
Maelezo haya ni amri ambayo iko wazi na inadai utekelezaji. Hivyo idara hii  iko kwa kusudi hili la kuhubiri Injili kwa watu wote na kupanda makansa katika maeneo mbalimbali, ndani na nje ya jimbo la Mbeya.
Tunaamini kwamba  uinjilisti na umisheni ndio kipaumbele cha kwanza cha Kanisa . Wosia wa mwisho wa Yesu Kristo kwa wanafunzi wake ulihusu Agizo kuu yaani Uinjilisti na umisheni. Matendo ya Mitume1:8
Wosia wa mwisho wa mtu huwa unashikwa na kufanyiwa kazi kuliko kitu kingine chochote kile. Hivyo kanisa linatakiwa kuupa uzito wa kipekee wosia  huu wa Agizo kuu.
Idara hii inalenga kuhamisisha  na kutumia rasilimali mbalimbali za kikanisa  kuanzia ngazi ya tawi, parishi na jimbo katika kuhubiri Injili  na kupanda makanisa yenye kujizidisha. Tunaamini raslimali kuu ni watu hivyo wamini wanatakiwa  kufanywa wanafunzi wenye uwezo wa kujizidisha ili kuufikia ulimwengu wote kwa Injili. Kuhakikisha watu wote wanafikiwa pale walipo kwa Injili ya Yesu Kristo.


Malengo mahususi
1.     Kuanzisha idara ya uinjilisi na umisheni  kuanzia tawini  hadi parishi.
2.     Kuandaa makongamano ya wahubiri na waimbaji  ili kupeana  uzoefu na changamoto katika huduma ili kuweza kuboresha huduma za waimbaji na wainjilisti walioko ndani ya KLPT  jimbo la Mbeya.
3.     Kuanzisha mfuko  wa jimbo wa huduma ya Uinjilisti na umisheni.
·       Kupendekeza asilimia tano (5%) ya mapato ya kila kanisa kuingia katika mfuko wa uinjilisti na umisheni.
·       Kuendesha halambee kwaajili ya kukuza mfuko wa Injili.
·       Kuanzisha miradi mbalimbali  mfano shule, gazeti, redio Nk
4.     Kuanzisha mtandao wa maombi  wa uinjilisti  na Umisheni.
5.     Kufanya uinjilisti wa Maandiko
Kuandaa vipeperushi, majarida na vitini kwaajili ya uinjilisti  wa maandiko.
6.     Kufanya Uinjilisti kupitia vyombo vya habari, mfano Redio, magazeti na  luninga.
7.     Kuanzisha tovuti ya idara
Kuanzisha tovuti ya idara ambayo itatumika kufaya uinjilisti kupitia mtandao.
Kufanya uinjilisti kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii
8.     Kukuza afya ya kanisa.
Kuhakikisha  makanisa yote ya KLPT Jimbo la Mbeya yanakuwa na vichocheo mbalimbali vitakavyosababisha  kukua kwa vipawa, karama na huduma za waamini wote na kuwafanya wanafunzi weye kujizidisha ili kuleta matokeo makubwa sasa katika uvunaji,  kwa kufanya yafuatayo .
·       Kila kanisa la mahali pamoja(tawi na parishi) kuanzisha ibada za maombi na maombezi ya nguvu kama chambo cha uvunaji.
·       Kuboresha mifumo ya ibada. Ibada zisikae kiburudani zaidi. Ibada zisigeuke kuwa ukumbi. Mambo ya kiroho yapewe kipaumbele zaidi katika ibada.
·       Uboreshaji wa majego na upatikanaji wa vyombo vya mziki na injili.





G.   Malengo ya idara kwa mwaka wa 2015
Idara hii imeweka mipango mikakati inayotakiwa kutekelezwa ndani ya mwaka wa 2015 kama ifuatavyo.
Kuanzisha idara ya uinjilisti mataiwini na parishi zote.
Utekekelezaji wake.
Viongozi wa idara hii watashirikiana na wachungaji wa makanisa husika katika kuanzisha idara ya Uinjilisti na Umisheni makanisani.
Utekelezaji wake ni kuanzia mwezi wa kwanza 2015 hadi mwezi wa tano 2015.
Kupanda makanisa mawili.
Kuandaa mikutano ya Injili  miwili  kuhubiri na kupanda kanisa katika vijiji/mitaa miwili katika jimbo la Mbeya. 
Utekelezaji ni Kuanzia mwezi wa sita hadi mwezi wa kumi na mbili 2015.
Kuanzisha tovuti ya Idara ya Uinjilisti na Umisheni.
Kufanya uinjilisti  kupitia mitandao ya kijamii, kama vile facebook, twiter n.k
Utekelezaji wake ni mwezi Januari 2015 na kuendelea.

Kuanzisha vipindi vya uinjilisti redioni.
Kuhakikisha angalau kwa mwezi tunakuwa na kipindi redioni.
Utekelezaji wake ni kuanzia mwezi wa tano na kuendelea.
Kuanzisha mfuko wa idara ya uinjilisti na Umisheni.
Kufungua akaunti , benki  kwaajili ya kutunza fedha za idara.
Utekelezaji wake ni mwezi Julai hadi Agosti 2015.

H.    Changamoto.
Idara hii ni mpya na imeanzishwa bila kuwepo maandalizi ya kutosha kwani inawawia vigumu viongozi wa idara kuongoza idara bila kuwepo mwongozo au maelekezo yenye kutoa mwanga wa uendeshaji wa idara.
Hivyo viongozi wanajikuta wanalazimika kuendesha idara kwa mfumo wanaouona wao unafaa. Idara imeanzishwa lakini hakuna muunganiko kati ya matawi, parishi, jimbo na taifa.
Tunaamini waanzilishi wa idara ndio wenye dira na maono ya idara hii. Hivyo kupewa kuongoza idara bila kupewa mwongozo ni kupewa kazi ya kuanzisha msingi juu ya msingi, jambo ambalo haliwezekani kiBiblia.
I.      Mapendekezo
Mapendekezo yetu kwa kamati tendaji ya jimbo na taifa kwa ujumla ni kwamba iandae mwongozo wa idara hii ili kuturahisishia utendajikazi.
Pia mfumo wa uongozi uboreshwe  kwa kuainisha viongozi  kimadaraka na majukumu  yao yaainishwe wazi kila mmoja.
Tunapendekeza mwongozo huo utakaoandaliwa uhusishe vitu vifuatavyo
·       Jina la idara
·       Malengo/makusudi ya idara
·       Nembo ya idara
·       Maono ya idara
·       Dira  ya idara
·       Muundo wa uongozi.
·       Sifa za viongozi
·       Majukumu ya uongozi kila mmoja
·       Muda wa kushika uongozi
·       Vikao vya uongozi
·       Vyanzo  ya fedha vya kudumu.
Kwa  msaada wa Mungu tutatenda  makuu,…..   Zaburi 60:12  




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni